Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

Cyprian Kizito Lwanga Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Kampala Amefariki

 Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki mjini Kampala Cyprian Kizito Lwanga amefariki akiwa na umri wa miaka 68, Kanisa limethibitisha

Katika taarifa iliyotolewa na Diyosisi ya Kampala ya Kanisa Katoliki, Askofu Lwanga alipatikana chumbani mwake akiwa amefariki Jumamosi asubuhi. Chanzo cha kifo chake hakijabainishwa.

Taarifa za kifo hicho cha ghafla zimewashtua Waganda wengi ambao wametumia twitter na WhatsApp kutoa rambirambi zao.

Mapema Ijumaa, aliongoza Wakristo katika ibaada ya Ijumaa njema akishirikiana na Askofu mkuu wa kanisa la Uganda Daktari Kazimba Mugalu,kupitia Baraza la Muungano wa Madhehebu ya Wakristo nchini Uganda (UJCC), ambalo alikuwa mwenyekiti wake.

Kizito Lwanga aliyetawazwa kuwa padri wa Kanisa Katolikio 1978 alionekana kama mkosoaji wa serikali ya NRM.

ALikuwa akiangazia wazi wazi dhidi ya ufisadi, ukiukaji wa haki za binadamu na marekebisho ya katiba ya nchi ili kuondoa ukomo wa muhula na urais ili kumruhusu Rais aliye madarakani, Yoweri Museveni kuongeza muda wa utawala wake.

Mwaka 2012 aliwahi kumuandikia barua Rais Museveni akimtaka astaafu ifikapo mwaka 2016.

Kifo chake kimepokelewaje?

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine aliandika katika mtandao wa Twitter: Nimepokea kwa mshtuko kifo cha ghafla cha Dkt. Cyprian Kizito Lwanga, Askofu Mkuu wa Kampala. Itakuwa vigumu kukabiliana na msiba huu.

Post a Comment

0 Comments