Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

MAANA YA MAJINA YA WATU WANAOANZIA NA HERUFI J, K, L, M, N

 Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "J"

Wana uwezo mkubwa wa kutoa mawazo bora, Huwa ni wafanyakazi bora sana hasa kutokana na uwezo wao wa kutoa mawazo pia wana uwezo mkubwa wa kusimamia jambo mpaka kutimia. Wanapenda marafiki, Wanapenda kufanya watu wanaowazunguka wana furaha muda wote, Huwa na tabia nzuri, Wanapenda sana kutoa na wengi huwa na uwezo mkubwa kifedha.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "K"

Huwa wakarimu na waaminifu sana, Huwa na sifa ya upatanishi, Wana aibu sana pia wanajua sana kujali. Wanapenda kufanya kazi kwa kikundi kwa sababu sio watendaji wazuri kama ukiwaachia wafanye kazi peke yao, Wana uwezo mkubwa kwenye biashara, Kwenye mapenzi hawana mzaha na wapo tayari kukaa muda mrefu bila kuwa kwenye uhusiano kumsubiri mtu wanaeona ni sahihi kwao.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "L"

Wanapenda sana kutoa, Wana uwezo mkubwa sana kwenye kuwasiliana (Communication) na huacha tabasamu kwa watu kila sehemu wanayopita, Ni mashabiki wazuri sana, Wengi hufanikiwa kwa kila jambo wanalofanya na huwa matajiri pia. Wakipenda wanapenda ukweli na humfanya mwenza wao kuwa mtu wa kwanza katika maisha yao kwa kila kitu, Wakitengana kwenye mapenzi wana uwezo wa kusahau haraka na kuingia kwenye uhusiano mwingine haraka.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "M"

Wanapenda kufanya vitu wanavyoona kwao ni sahihi hivyo huwa wagumu sana kufuata ushauri wa watu wengine, Huwa na tabia ya ubinafsi, Wanapenda kuona wapo sahihi kwa kila ubishani unapotokea. Ni wachapakazi sana, Wanajiamini, Wanapenda sana pia kukaa nyumbani, Kutokana na tabia zao za ubinafsi huishia kutanga tanga' sana kuanzia kikazi mpaka kwenye mahusiano.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "N"

Wabunifu sana, Ni watatuzi wakubwa sana wa shida mbalimbali sababu wana uwezo mkubwa wa kufikiria nje ya Box', Wanapenda sana uhuru na Hawapendi kabisa kufuata ratiba/taratibu. Kutokana na tabia yao ya kupenda kuwa huru huwa hawadumu sana kwenye kazi na hata pia kwenye mahusiano.

Post a Comment

0 Comments