Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

MAANA YA MAJINA YA WATU WANAOANZIA NA HERUFI O, P, Q, R, S, T

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "O"

Ni wachapakazi na wakiamua kufanya jambo huhakikisha mpaka linatimia, Huwa na maadili mema na huhakikisha wanafuata njia zao kwa ukamilifu bila kuharibu jambo lolote, Wanapenda sana usawa na haki. Wanapenda kufuata sheria na taratibu, Huamini kuhusu masuala ya kiimani, Wanaamini sana kwenye mahusiano hivyo ni nadra kukuta anakuwa singo' kwa muda mrefu, Huwa na shauku sana hali ambayo huwafanya kuonekana kuwa na wivu kupitiliza.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "P"

Wengi huwa ni wasomi, Wanapenda kuonekana wamefanikiwa kwa jambo lolote hali hiyo imepelekea wengi kujikuta wanafanya kazi zenye ujuzi maalum, Wanajali sana kuhusu muonekano sio wao tu hata kwa watu wengine, Kama wataona kuna mtu hana faida nzuri kuhusu namna wanavyoonekana pamoja basi haraka hujitenga mbali. Mara nyingi uhusiano wao kimapenzi huwa wenye hali tete tu, Ugomvi kidogo unaweza pelekea penzi kuvunjika mara moja.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "Q"

Muda wote wapo tayari kwa jambo lolote (Active), hawapendi kukaa tu bila kazi kwa ufupi ni watendaji wazuri wa kazi, Huwa Hawaeleweki eleweki kirahisi. Wanatengeneza pesa kirahisi sana ila huwa wanapata sana tabu kwenye matunzo ya pesa, Wanapenda kufanya kila jambo wao tu. Wanapenda kupendwa na pia wakiwa kwenye mahusiano hupenda kupewa zawadi kama Maua, Chocolate n.k. Wanateseka sana kwenye mahusiano hivyo huishia kutoka kimapenzi na watu wengi na mwisho huachwa.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "R"

Hawa muda wote wanapenda kukubalika tu, Hupambana sana ili kuwa bora zaidi kwenye jambo wanalofanya. Wana hisia sana, Wapo tayari kujifunza na kubadilika yote ni kutokana na tabia yao ya kupenda kukubalika. Wana nguvu sana ya utendaji kwenye kazi, Wanapendwa/ Na wengi hufanya kazi kwenye vitengo vya usalama, Wanapenda kuwa kwenye uhusiano na watu ambao wanafanana kama wao, Ni wakarimu sana pia.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "S"

Wanapenda sana kutoa, Huwa ni wakarimu sana, Wana hisia pia kiasi kwamba kuna muda huonekana kama ni watu wa Drama' nyingi hasa kwenye mapenzi. Wanajiamini na huwa wabunifu, Wapo tayari kukaa singo' kwa muda mrefu ili kumsubiri mtu ambae wanaona ni sahihi kwao, Wapo serious' sana kwenye uhusiano, Wakipenda ni wanapenda kweli. Wana wivu sana hasa kutokana na tabia yao ya kupenda kuonesha umiliki.

Post a Comment

0 Comments