Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

MAANA YA MAJINA YA WATU WANAOANZIA NA HERUFI F, G, H, I,

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "F"

Hawa wanajua sana kujali, Wapo tayari kujitoa sadaka kwa tatizo lako, Wanapenda marafiki, Wacheshi, Wanapenda sana amani. Wanapenda kuinua watu wengine, Hupenda kusaidia watu wenye shida mbalimbali, Huwa na machale' sana, Wanajua sana mahaba, Wanapenda kudeka/kubembelezwa na wakipenda wanapenda kweli, Ukiwaumiza wanapenda kulipa visasi.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "G"

Hawa wao wanapenda kufanya kila jambo kwa usahihi hali inayopelekea kuwa wagumu sana kunyenyekea, Huwa na itikadi kali kwa wanachoamini pia wanapenda sana kusoma historia na kusafiri. Wana maono ya mbali, Wanapiga sana kazi, Hawapendi bughuza wakiwa wanafanya kazi, Wapo tayari kuwa wapweke (Lonely) kwa muda mrefu kuliko kuwa kwenye uhusiano ambao wanaona hauna faida kwao, Ni nadhifu sana katika mambo mengi.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "H"

Huwa wana bahati yakupata pesa nyingi lakini huzipoteza kwa haraka pia, Ni wabunifu, Ni ngumukuwabadilisha kwa kile wanachoamini, Ni wavumilivu pia wakarimu. Huwa wanajionakama hakuna umuhimu wa kuwa kwenye uhusiano maana wanapenda kuweka mipango yaombele muda wote hivyo huishia kutoka kimapenzi na wengi.

Watu ambao majina yao ya mwanzo huanzia na herufi "I"

Wanapenda kujifunza na kujaribu vitu vipya, Ni wabunifu sana hususani kwenye ulimwengu wa mitindo, Ubunifu wa ndani na Muziki. Husumbuliwa sana na huzuni mara kwa mara yote ni kutokana na tabia yao ya kupenda kubuni, Wanakasirika kasirika kwa vitu vidogo, Wanapenda kupokea sana zawadi kutoka kwa wenza wao, Wanapenda kujaliwa sana hali inayopelekea kushindwa kudumu kwa kipindi cha muda mrefu kwenye mapenzi.


Post a Comment

0 Comments