Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

Mazishi ya Prince Philip yaadhimisha 'uaminifu thabiti' kwa Malkia huku watu wakitikwa a machozi wakikumbuka uka....

 ''Uaminifu usioyumba wa Mtawala wa Edinburgh kwa Malkia, huduma kwa taifa na "ujasiri", vitaadhimishwa katika mazishi yake baadae leo.

Uhusiano wa Mwanamfalme Philip na jeshi la wanamaji - Royal Navy na mapenzi yake ya bahari vitaangaziwa katika sherehe ya maazishi yake itakayofanyika katika Kasri ya Windsor.

Lakini hakuna mahubiri yatakayotolewa , kulingana na matakwa yake.

Zaidi ya wanajeshi 730 wanashiriki katika tukio hilo, lakini kuna ukomo wa watu 30 pekee watakaohudhuria misa hiyo katika kanisa dogo St George, chini ya sheria za Covid.

Mazishi hayo ya sherehe za kifalme yatatangazwa na televisheni ya BBC One, huku taarifa kuhusu mazishi hayo zikiendelea kutangazwa moja kwa moja Misa yenyewe itaanza baada ya dakika moja ya taifa kukaa kimya T saa tisa kwa saa za Uingereza.

Mwanamfalme Philip alikufa katika kasri la Windsor siku ya Ijumaa tarehe 9 Aprili, akiwa na umri wa miaka 99.

Mwili wake kwa sasa umelazwa katika ukumbi wa ndani katika Kasri la Windsor baada ya kuondolewa kwenye kanisa dogo la kibinafsi.

Jeneza lake litawekwa katika gari lililorekebishwa la Land Rover ambalo Mwanamfalme Philip mwenyewe alisaidia kuliunda na kubebwa kwenye msafara mfupi wa kuelekea katika kanisa dogo la St George kwa jili ya ibada

Misa ya mazishi itaongozwa na mtaalamu wa masuala ya Winsor, huku Askofu Mkuu wa Canterbury akitangaza baraka.

Mpangilio wa ibada hiyo, uliotolewa na kasri la Buckingham , inasema Mtaalamu wa Windsor atatoa risala kwa Mwanamfalme Philip kuhusu "ukarimu, ucheshi na utu" wake na " kwa jinsi maisha yake marefu yalivyokuwa baraka kwetu".

" Tumehamasishwa na na uaminifu wake thabiti kwa Malkia wetu , huduma yake taifa na Jumuiya ya Madola, kwa ujasiri wake, na imani ," atasema wakati wa risala.

Kasri ya Buckingham imesema mipango ya mazishi imebadilishwa kuzingatia miongozo ya afya ya umma.

Mazishi yatafanyika kikamilifu ndani ya uwanja wa kasri na umma umeulizwa usikusanyike huko au kwenye makao mengine ya kifalme.

Watakaohudhuria watavalia maski na kutokaribiana kwa mujibu wa kanuni za kupambana na Covid, na Malkia ameketi peke yake.

Lakini mambo ya sherehe ya siku hii na huduma nzima ya misa ya mazishi yake yatasalia sambamba na matakwa ya Prince Philip na itaonyesha uhusiano wake wa karibu na jeshi na mambo ya kibinafsi ya maisha yake.

Muziki utajumuisha wimbo wa 1860 Baba wa Milele, Nguvu ya Kuokoa, na William Whiting, ambazo iznahusishwa na mabaharia wa huduma za jeshi la baharini.

Kabla ya mazishi, Malkia alitoa kwa umma picha anayopenda mwenyewe na Duke wa Edinburgh, ikionyesha wakiwa huko Aberdeenshire.

Picha hiyo ilipigwa na Countess wa Wessex mnamo 2003, picha inaonyesha Malkia na mumewe wakipumzika katika uanja mdogo wa nyasi kwenye eneo la kuvutia Coyles of Muick, karibu na nyumba ya kibinafsi ya Malkia ya Balmoral.

Watoto wanne wa Malkia na duke Mwanamfalme wa Wales, Princess Royal , Duke wa York na Earl wa Wessex na - vile vile wajukuu wao wanane - watahudhuria, lakini hakuna vitukuu wao watakaohudhuria

Wanandoa wa watoto wao pamoja na wa wajukuu wao watakuwa katika msafara wa waombolezaji wakiwemo wawili ambao wamefunga ndoa na wanawafalme katika miaka ya hiviri karibuni - Jack Brooksbank na Edoardo Mapelli Mozzi, waume za wanawafalme Eugenie na Beatrice.

Lakini mkewe Mtawala wa Sussex, Duchess wa Sussex, yupo mja mzito na ameshauriwa na madaktari kutposafiri kutoka Marekani

Waombolezaji wengine ni watoto wa dadake Malkia Princess Margaret, na jamaa watatu Wajerumani wa Prince Philip - Bernhard, Mrithi wa kifalme wa Baden; Donatus, Prince na Landgrave wa Hesse; na Prince Philipp wa Hohenlohe-Langenburg.

 

Post a Comment

0 Comments