Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

Namna ya Kutengeneza Tomato sause Nyumbani bila Kifaa Chochote.

 

Utangulizi Namna ya Kutengeneza Tomato sause Nyumbani .

v  Sosi ya nyanya ni kiungo kinachotumika ili kukoleza chakula wakati wa mlo. Sosi ya nyanya hutengenezwa kutokana na nyanya zilizoiva na ni viungo.

v  Jinsi ya kutengeneza:

v  Vifaa vinavyohitajika:

v   Mashine ya kusagia

v  Sufuria ya kuchemshia

v   Mzani

v  Vifungashio:- Chupa za sosi zenye mifuniko

v  Mahitaji:

v  Nyanya zilizoiva gramu 900

v  Siki (vinegar) mls 50

v  Sodiumu Benzoate

v  Maji salama

v  Vitunguu maji, vitunguu swaumu, hoho ya unga, haradani (mustard n.k)

v  Chumvi

v  Sukari

v  Unga wa muhogo 1-1.3%

v  Hatua za Utengenezaji:

v  Chagua nyanya zilizoiva vizuri zenye umbo la yai- nyanya za Tengeru ni nzuri zaidi.

v  Osha kwa maji safi

v  Menya na kuondoa mbegu (waweza pia pika na mbegu ingawa kuna wengine huwa hawapendi ladha na muonekano wa mbegu kwenye sosi)

v   Katakata vipande vidogo na weka kwenye chombo cha kusagia.

v  Saga vizuri kupata rojo

v   Visage viungo( vitunguu, hoho, pilipili manga, vitunguu swaumu, binzari n.k kulingana na matakwa) na vifunge kwenye kitambaa safi.

v   Kitumbukize kwenye maji kiasi na chemsha na kamua kitambaa ili kupata supu

v   Changanya supu ya viungo, chumvi, sukari na mchanganyiko wa nyanya Chemsha mpaka upate uji mzito. Mara nyingi sosi inakua tayari iwapo uzito umebaki nusu ya uzito wa mchanganyiko wa awali.

v  Ongeza kamikali (Sodium Benzoate, Vinegar) kisha chemsha kwa dk 5

v   Paki kwenye vifungashio safi ikiwa bado ina joto nyuzijoto 80-90

v  Vifungashio na lebo

v  Fungasha bidhaa yako kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua

v  Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa: Aina, uzito au ujazo, mwisho wa matumizi, maelekezo ya matumizi, uhifadhi na mchanganyiko wa malighafi/lishe, jina na anwani ya mtengenezaji, namba ya simu na barua pepe

v  Onyesha nembo za ubora kama TBS, TFDA na GS1 (Barcode)

v  Fuata maelekezo na taratibu za TFDA na TBS

v  Hati na vibali

v  Onana na mamlaka husika kupata vyeti: TFDA, TBS and GS1

v  Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi

v  Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi

Endelea kuwa nasi dinony.online Mautundu........................

Post a Comment

0 Comments