Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

TANZANIA IMETISHA KWA KUANZISHA BEI MPYA YA VIFURUSHI HUKU TCRA WAKISEMA NA BAD......

 Tanzania yasitisha bei mpya ya vifurushi vya data

Watumiaji wa mitandao ya simu nchini Tanzania wamepata ahueni japo ya muda baada ya serikali kusitisha kutumika kwa bei mpya za vifurushi, hadi suala hilo litakaposhughulikiwa.

Tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya siku ya Ijumaa, mjadala mkali umeibuka katika mitandao ya kijamii kupinga hatua hiyo huku baadhi ya watumiaji wa mitandao ya simu wakielezea masikitiko yao kwani walitarajia kushuka kwa gharama hizo.

"Tumesitisha matumizi ya gharama mpya za vifurushi hadi hapo itakapotangazwa baadaye. Lakini, hili litahusu vifurushi vya data pekee na vile vya sms na kupiga vitaendelea kama kawaida," Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, alinukuliwa na na gazeti la Mwananchi.

Mnamo tarehe tano mwezi Februari, TCRA ilitoa tangazo la kuzingatia maoni ya wadau kuhusu huduma za vifurushi zinazotolewa na watoa huduma za mawasiliano za simu za mkononi.

Mapema mwezi Machi, 2021 TCRA,iliahidi utekelezaji wa kanuni hizo za kukabiliana na malalamiko juu ya huduma ya vifurushi yaliyotokana na maoni 3, 278 yaliyotolewa na wananchi.

''Kutokana na maoni hayo iliandaa kanuni za vifurushi za 2021 kwa lengo la kuweka utaratibu kwa watoa huduma wa namna ya kupanga, bei na muda wa matumizi hivyo. Kanuni hizi zilianza kutekelezwa Aprili tarehe mbili'', TCRA ilisemakatika taarifa yake.

Watumiaji wa huduma za simu wamekuwa wakilalamikia gharama za vifurushi kuwa juu na vifurushi vya data kubadilika mara kwa mara.

Siku ya Alhamisi mitandao ya simu iliwataarifu watumiaji wake juu ya mabadiliko hayo, lakini kilichowashangaza watumiaji wa huduma hiyo ni kuminywa kwa vifurushi hivyo kinyume na ilivyokuwa awali wakati walipotoa malalamiko hayo.

 

Post a Comment

0 Comments