Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 06.04.2021: Haaland, Sancho, Messi, Salah, Ibrahimovic, Foyth.

 Wakala Mino Raiola amekana tetesi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,20. (Goal)

Mtendaji Mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amesisitiza kuwa klabu yake inapanga msimu ujao na Haaland. (Dazn via Mirror)

Hatahivyo, anasema klabu hiyo itasikiliza ofa kwa ajili ya winga wa England Jadon Sancho. (Manchester Evening News)

Kocha Pep Guardiola amesema Manchester City wanaweza kuamua kutumia zaidi ya pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji mmoja siku za usoni, lakini ameendela kuwa na kigugumizi juu ya tetesi kuhusu klabu yake kuhusishwa na Haaland. (Sky Sports)

Simba yatinga Robo Fainali Afrika kwa kishindo

Barcelona itaendelea na mipango yake ya kumnada mchezaji huyo wa Norway baada ya kukutana na wawakilishi wake wiki iliyopita, lakini vyanzo katika klabu hiyo wanasema kuwa itakuwa''vigumu sana'' kutekeleza azma yao. (ESPN)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amevunja ukimya ukimya kuhusu tetesi za uhamisho zinazomuhusisha mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah,28, kuhamia Bernabeu. (Liverpool Echo)

Villarreal wana matumaini ya kumsajili mlinzi Juan Foyth,23, wa Tottenham msimu huu kwa mkataba wa kudumu kwa kiasi cha chini ya ada ya pauni milioni 13.Kwa sasa mchezaji huyo anacheza kwa mkopo katika klabu hiyo.(Football Insider)

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 05.04.2021

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Angel di Maria, 33, amesema itakuwa ''vizuri sana'' kucheza na Muajentina mwenzake Lionel Messi,33, wakati kukiwa na mashaka kuhusu mustakabali wake ndani ya Barcelona. (AS)

Mmiliki mwenza wa zamani wa Roma na mwenyekiti James Pallotta ameeleza shauku yake ya kununua klabu ya primia akiitazama New Castle United. (The Athletic)

Mshambuliaji wa Uswidi Zlatan Ibrahimovich, 39, anajiandaa kusaini nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja na AC Milan. (Sky Sports)

Norwich City itamtunza raia wa Norway Alex Tettey chochote kile kuhusu mustakabali wake kiungo huyo wa miaka 35 Tettey amekuwa Norwich tangu 2012 na mkataba wake unamalizika msimu wa joto. (Norwich Evening News)

Post a Comment

0 Comments