Ad Code

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA 0745507517.

UMOJA WA MATAIFA UNAKUMBUKA MCHANGO WA RAISI MAGUFULI KATIKA MIJADALA YAO.

 Baadhi ya viongozi katika kikao cha 75 cha mkutano wa 59 wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika siku ya Ijumaa Aprili tarehe 16, 2021 wametambua alama za uongozi za za aliyekuwa rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli.

 

Viongozi hao wameahidi kuendelea kushirikiana na rais wa sasa wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan .

Kikao hicho kiliongozwa na Volkan Bozkir Rais wa baraza kuu la UN kilikuwa na ajenda kadhaa ikiwemo ya kutambua mchango wa Magufuli aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021.

Katibu mkuu wa umoja huo, António Guterres amesema Magufuli atakumbukwa kwa mchango wake katika kurejesha maadili ya utumishi wa umma, kupambana na rushwa, ujenzi wa miundombinu na mapinduzi ya viwanda ambayo ni msingi katika ukuaji uchumi.jamiiway.com

"Tanzania imefanikiwa kufikia nchi ya watu wenye kipato cha kati miaka minne kabla ya kufikia 2025, alifanikiwa kuwezesha mfumo wa elimu bila malipo iliyowezesha watoto wengi kuongezeka shuleni, pia alifanikiwa kupeleka huduma za umeme vijijini kwa jitihada za kufikia wananchi wengi." Imesema taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Umoja wa Mataifa.jamiiway.com

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa amesema awamu ya 5 ikitamatika tarehe 17 mwezi Machi mwaka huu wa 2021, ukurasa mpya ulifunguliwa wa awamu ya 6 tarehe 19 Machi 2021 kwa kuapishwa kwa Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama.

"Tunajivunia kama taifa na tunashukuru kwamba katika hatamu za uongozi, kwa mara ya kwanza tuna Mwanamke ambaye ni Mkuu, ikiwa ni historia. Rais Samia ni mzalendo na mwanasiasa anayezingatia misingi, ana maono na muumini na muungaji mkono wa ushirikiano wa kimataifa," amesema Profesa Gastorn.jamiiway.com

Chini ya uongozi wake, Tanzania itaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Umoja wa Mataifa na misingi yake ambayo ni amani na usalama duniani, haki za binadamu, maendeleo na ustawi wa binadamu, "Rais Samia tayari amechukua hatua za kiuongozi kwa unyenyekevu na ubunifu, kasi na upendo katika kufanikisha ajenda 2030 ya maendeleo endelevu."

"Kwa niaba ya umoja wa mataifa ninatoa pole kwa familia, natumia nafasi hii kuahidi umoja wa mataifa kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali iliyopo chini ya Samia Suluhu Hassan, tuko pamoja na raia wa Tanzania katika juhudi zao za kujiletea maendeleo," amesema Guterrez.

Mwakilishi kutoka Ulaya Magharibi, amesema rais Magufuli alikuwa kiongozi aliyejitoa kwa ajili ya kuwaletea Watanzania maendeleo na kwamba juhudi zake zilitambulika kwa kiwango kikubwa kupitia sekta ya elimu na miundombinu.jamiiway.com

Kutambuliwa kwa Magufuli katika ulingo huo wa kimataifa kunajiri wakati huu ambapo pia alama zakea zinajadiliwa nchini humo ikiwemo katika bunge ambapo kunao wanaotaka yote aliyoyaanzisha yasibadilishwe ilhali wengine wana maoni tofauti kuhusu mwelekeo unaofaa kuwa wa nchi hiyo chini ya rais Samia.

Mjadala wa Alama za Magufuli bungenijamiiway.com

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akitoa maoni yake kuhusu mjadala huo siku ya ijumaa alisema alama aliyoacha ya kiongozi haitetewi, bali inajitetea yenyewe.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri na kwamba yeye kama awamu nyingine za uongozi, "aachwe aandike kitabu chake cha awamu ya sita".

Nape alisema kama ilivyokuwa kwa awamu nyingine zilivyofanya maboresho katika maeneo mbalimbali, naye kama atahitaji kufanya hivyo asaidiwe ili kazi ifanyike.jamiiway.com

Aliwaomba viongozi, wabunge na Watanzania kwa ujumla wampe ushirikiano Rais Samia ili aweze kuyafanya hayo.

 

 

 

Post a Comment

0 Comments