KANUNI ZA KUFANIKIWA KUTOKA KATIKA UCHUMI MDOGO KWENDA UCHUMI MKUBWA

Utangulizi:

• Tunaishi katika nyakati ambazo ili mtu aweze kuyamudu maisha vizuri, anahitaji kuwa na vyanzo kadhaa vya kimapato na sio chanzo kimoja.

 • Ujasiliamali ndio moja ya ndio kitu kitakachoweza kuleta suluhisho la kiuchumi na kuboresha maisha ya mtu. •

 Kuongeza kipato zaidi ya mshahara unao upata. KANUNI ZA KUFANIKIWA KIUCHUMI 1. Mafanikio ya kiuchumi/kibiashara hayaanzii kwenye kuwa na mtaji – bali maarifa ya biashara yenyewe.

• Kabla hujatafuta mtaji wa biashara unayotaka kuifanya, tafuta kwanza maarifa ya juu ya hiyo biashara unayotaka kuifanya.

• Mitaji ya watu wengi imeteketea kwasababu walianza kutafuta mtaji wa biashara kabla ya kutafuta maarifa juu ya biashara anayotaka kuifanya.

• Usichukue taarifa za mtaani ukaenda kukopa mtaji uanze biashara. Mtaji utapotea na utabaki kulipa deni la mtaji ambao haukufanikisha lengo – That is called a step back. 2. Mafanikio ya kiuchumi/biashara yanategemea kiwango cha usimamizi wa biashara au kitegeuchumi hicho.

• Ni nani unayemuweka kusimamia hiyo biashara. i. Usitafute watu na kuwapa usimamizi wa biashara kwa Misingi ya Undugu au Urafiki unless anao ujuzi na uwezo huo wa jukumu hilo. ii. Usitafute watu na kuwapa usimamizi wa biashara kwa Misingi ya Ukabila. iii. Usitafute watu na kuwapa kazi au majukumu kwa Misingi ya Kumuhurumia Mtu.

 

Kwao wazazi wake wote wamekufa kwahiyo ngoja tu tumpe hii kazi hata kama hajasomea.

Huyu ni mjane anamzigo mkubwa wa watoto nyuma yake ngoja tu ajibanze hapa asogeze siku.

  Huyu alizalishwaga sana na wanaume wote wakamkimbia sasa ngoja tu tumpachike hapa naye yeye apate pate chochote cha kumsaidia. 3. Mafanikio ya kiuchumi/biashara yanahitaji Nidhamu ya Fedha na Matumizi. Note: Kinachofanya watu wengi washindwe kufikia ndoto za mafanikio ya uchumi na maisha yao ni tatizo la matumizi mabaya ya fedha yasiyo na nidhamu

. • Jifunze kuweka akiba

  Fungua akaunti hata kama kipato chako ni kidogo.

  Usisubiri mpaka utakapokuwa tajiri ndio utaanza kuweka akiba.

Usisubiri mpaka utakapokuwa umepata vingi ndipo uanze kuweka akiba.

 • Watu waliofanikiwa sana katika maisha ni wale waliojitahidi kujinyima na kujijengea mazoea ya kuweka akiba kidogo kidogo. (Accumulation)

 • Ukipata pesa wekeza kwanza kisha kula kinachobaki. Tofauti ya Masikini na Tajiri

  Masikini akipata pesa anakula kwanza kisha anawekeza kama itakuwa imebakia.

Tajiri akipata pesa anawekeza kwanza kisha anakula inayobaki.

• Epuka kukopa kwa shughuli isiyo ya maendeleo.

Jiepushe na kukopa kopa vitu kutoka kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wanaokopesha vitu mbali mbali ambavyo sio vya muhimu. Usikope kwajili ya harusi – tafuta michango na ukipata kidogo fanya harusi ndogo kulingana na kipato chako usitake mambo makuu yatakuumiza.

Usikope kwajili ya sherehe kama birthday, graduation nk.

Ukikopa iwe ni kitu cha kimaendeleo.

• Jifunze kuweka vipaumbele juu ya mahitaji muhimu utakayo fanya kwa pesa iliyopo mkononi mwako.

Usijaribu kutaka kutekeleza kila hitaji.

Mahitaji ni mengi hutaweza kuyamaliza.

Michango ni mingi hutaweza kumchangia kila mtu.

Madeni ni mengi hutaweza kuyalipa yote kwa mara moja.

Sio kila unacho kitaka ni lazima ukipate.

There is difference bebween what you want and what you need. • Usikope vitu ambavyo vitakuwa vinakunyonya Zaidi badala ya kukuingizia kipato.

Mfano unakopa gari la kutembelea tu ambalo sio la lazima na halikuingizii kitu na huna uwezo wa kulihudumia.

  Usikope gari huku huna uhakika wa mafuta au kulihudumia.

  Mahitaji ya gari ni kama mahitaji ya mwanadamu tu:

Gari linahitaji kula na kunywa.

Gari linahitaji kuoga.

Gari linahitaji kwenda hospitali mara kwa mara.

Gari linahitaji kulipiwa kodi na ushuru wa mara kwa mara. Kama unakipato kidogo na hujafanya mambo mengine ya kipaumbele, usitangulize kukopa gari kwanza na hasa gari ambayo sio ya kukuongezea kipato.

 • Usipende kukaa na fedha mfukoni, nyumbani au kwenye simu zako. Jitahidi uwe na akaunti yako na kila mara tupia huko chochote kinachoingia. Mkononi ibaki pesa kidogo tu ya matumizi madogo madogo.

  Usipende kutembea na ATM card yako kila unapokwenda.

• Usimpe pesa Rafiki yakow ala ndugu yako hata kama ni mzazi wako au kaka au dada akuwekee ili siku ukiwa unazihitaji akupe. Pesa zako zitunze mwenyewe. Fungua akauti yako fungia pesa zako huko.

Mtaharibu Urafiki wenu,

Mtaharibu undugu wenu. 4. Dhibiti vyanzo vyako vya msongo wa mawazo

 • Msongo wa mawazo unamchango mkubwa sana katika kuudhohofisha uchumi wa mtu

. • Msongo wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu kufikiri kwa kina.

 • Msongo wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu wa ubunifu.

• Msongo wa mawazo unapunguza uwezo wa mtu katika kufanya maamuzi. How:

• Ishi kwa kiwango chako

Social involvement

• Let your feelings out – Kucheka au Kulia.

• Kula chakula kizuri pale inapowezekana.

• Lala mahari Pazuri – Mahali unapolala pana uhusiano mkubwa sana na kiwango cha Stres.

 • Pata rafiki mzuri unayemwamini wa kumshirikisha mambo yako na hasa yale yanayo kuumiza usibaki nayo moyoni.