Biashara ya Mtandao na Nguvu zake Katika Kukuza Kipato

Kama tulivyoona katika utangulizi hapo juu,biashara ya mtandao inahusisha usambazaji wa bidhaa au huduma ili kuwafikia watumiaji toka mtu mmoja kwenda kwa mwingine.Kwa kiasi kikubwa hii hufanyika kwa njia ya mdomo toka kwa mtu ambaye anatumia bidhaa au huduma kwenda kwa mwingine. Uaminifu na mahusioano mazuri ndio msingi wa biashara ya mtandao.

Nguvu ya Biashara ya Mtandao katika Kipato

Biashara ya mtandao inatoa nafasi kubwa katika kuanza na kukuza biashara yenye kukupa faida katika muda mfupi sana.

Zifuatazo ni baadhi ya faida kubwa za biashara ya mtandao:

Unaweza kuanza na Mtaji Mdogo: Biashara ya mtandao ndio biashara pekee unayoweza kuanza kwa mtaji mdogo sana na yenye uwezo wa kukupa faida kubwa katika muda mfupi. Makampuni mengine unaweza ukaanza hata kwa Tsh 100,000 tu na mengine yana viwango vya juu zaidi.

Uwezo wa kupata Faida Katika Muda Mfupi: Unaweza ukapata faida katika mwezi mmoja tu kulingana na mfumo ambao kampuni inautumia na juhudi unazoweka katika kujenga timu chini yako.  Shida ya wengi katika biashara hii hasa katika nchi za afrika ni kuwa hatuichukulii kama biashara na hivyo kuipa umuhimu mdogo sana. Tunafanya kazi kwa muda mfupi sana, wengine hawaweki hata saa moja katika wiki nzima kitu ambacho kinasababisha kupata matokeo hasi.

Muda Mfupi wa Kazi: Katika biashara hii huhtaji kufanya kazi masaa 8 kama katika ajira. Masaa 2-4 kwa siku yanaweza kukupa matokeo mazuri sana hivyo kutumia muda uliobaki katika siku kufanya mambo mengine ikiwemo kukaa na familia yako au kusafiri.

Kutumia Nguvu ya Watu: Mafanikio katika biashara ya mtandao yanakuja kwa kujenga timu ya watu wanaotumia bidhaa za kampuni husika. Na kufundisha ,na kuhimiza kila mmoja katika timu yako kufanya hivyo hivyo kama unavyofanya wewe. Hii inakufanya usitumie nguvu nyingi sana kupata kipato kama katika kazi nyingine za kujiajiri ambapo mara nyingi inategemea uwepo na nguvu za mtu mmoja.

Uwezo wa Kupata Fedha Nyingi: Biashara hii inauwezo wa kukupa kipato kikubwa katika muda mfupi. Katika muda wa miaka 3-5 uanweza ukapata fedha nyingi sana ambazo huwezi kuzipata katika kazi ya kuajiriwa au hata ajira binafsi na biashara ndogo yoyote. Inakupa uwezo wa kupata hata Tsh Bilioni 1 katika muda wa mwaka mmoja kulingana na kampuni na mfumo unaotumika ka kampuni husika.  [Soma namna ya kutengeneza Tsh Bilioni 1.6 kupitia Biashara ya Mtandao Katika Mwaka 1]

Kwa hiyo kama mtu anataka kukua kiuchumi haraka,biashara ya mtandao ni sehemu muafaka kufikia malengo yake kwa haraka na kuondokana na umasikini.

Lakini ni muhimu kutambua kwamba biashara ya mtandao sio njia ya kuwa tajiri kwa haraka bila ya kufanya kazi. kazi inahitajika hasa katika mwaka wa kwanza unapojenga biashara.

Nguvu ya Biashara ya Mtandao na Intaneti Katika Kukuza Masoko

Tumeona kuwa vyote intaneti na biashara ya mtandao vyote vina nguvu kubwa kwa namna tofauti.

Nguvu ya intaneti ipo katika kusambaza habari kwa haraka na urahisi bila kujali mopaka ya kijiografia na nguvu ya biashara ya mtandao ipo katika kuwezesha kusambaza bidhaa toka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa gharama ndogo na kwa ufanisi mkubwa.

Ukijumuisha vitu hivi viwili yaani intaneti na biashara yamtandao utapata matokeo makubwa sana katika mauzo ya bidhaa za kampuni husika.

Unapotumia intanneti kuweza kuwafikia watu wengi juu ya biashara unayofanya unapata wateja wengi au watu wengi watakaoona fursa yako na katika hao wengi pia baadhi yao watajiunga na kununua bidhaa toka katika kampuni yako.

 Hapa intaneti  inamwezesha mwanamtandao kuweza kuwafikia watu wengi wengi ambao anaweza kuanzisha mahusioano nao na hatimaye wakfanya biashara. Mfano mtu anaweza akakutana na mtu mwingine katika mtandao wa kijamii kama facebook au twitter kisha wakajenga mahusiano na baadae wakafanya biashara.

Ukiangalia  hapa hakuna mipaka kwa mtu mmoja ambaye yupo katika biashara ya mtandao katika kuwafikia watu. Hii ndio nguvu ya kufanya boahsra ya mtandao katka intaneti.

Namna za kuwafikia Watu Kupitia Intaneti:

Mitandao ya Kijamii: Matumizi ya facebook,twitter,instagram,pinterest etc  kukutana na kujemga uhusiano nao ambao baadae wanaweza wakawa wateja katika kampuni yako ya mtandao.

Blogu na Tovuti: Tovuti na blogu inawezesha taarifa kuwafikia watu duniani kote. Blogu ni bora zaidi katika kufikisha taarifa nahupendwa sana na watu kutokana na habari zake kubadirika mara kwa mara

Barua Pepe: Ukiwa na anuani nyingi za barua pepe unaweza ukatuma matangazo ya fursa ya biashara yako na kuwafikia watu wengi kwa mara moja. Baadhi yao kati ya hawa watapenda na kujiunga na fursa yako.

Mikutano ya Mbali: Badala ya kukutana na watu ana kwa ana katika mikutano sasa hivi unaweza kufanya mikutano kupitia mtandao wa intaneti hivyo kuondo kiwazo cha wapi mtu au watu walengwa wapo.

Kupitia njia zilizotajwa mwanamtandao anaweza kupata wateja wengi kupitia intaneti.

Kampuni Inayouza Bidhaa Kupitia Mtandao kwa 100% Na namna ya Kujiunga

Makampuni mengi ya biashara ya mtandao yanajitahidi kutumia intaneti, mfano kwa kuelimisha watu na hata kuonesha na kuuza bidhaa zao.

Kampuni ya QNET ni mojawapo ya makampuni machache yanayotumia intaneti kwa 100%. Kampuni hii inaonesha bidhaa na kuziuza mtandaoni hivyo kuwezesha wanachama wake kumilki duka la bidhaa na kuzitangaza duniani kote kupitia tovuti ya kampuni.

Kama unataka kutumia nguvu ya biashara ya mtandao na intaneti basi pata taarifa zaidi kuhusu kampuni hii na ujiunge. Pata taarifa zaidi kuhusu QNET na jinsi ya kujiunga.

[Kwa maswali kuhusu fursa ya QNET wasiliana nami kupitia Whatsapp: 0745507517 au SMS/Piga 0745507507 nitakueleza namna ya kufanikiwa katika Biashara ya Mtandao na Intaneti]

Hitimisho:

Mafanikio makubwa katika biashara leo yanaweza kupatikana kama utatumia intaneti. Biashara ya mtandao hali kadharika ni mojawapo ya biashara ambayo kupitia intaneti inakupa nafasi ya kupata watu wengi watakaonunua bidhaa toka katika kampuni yako inayotumia biashara ya mtandao.

Kama wewe upo katika kampuni ya biashara ya mtandao basi anza leo kujenga biashara yako kupitia intaneti ili uweze kufaidika ma nguvu ya intaneti katika kukuza biashara na kipato chako.

Kama umeipenda makala hii juu basi washirikishe na wengine ili wafahamu juu ya Nguvu ya Biashara ya Mtandao na Intaneti kuweza kujipatia kipato. Kama una mawazo ,hoja au maswali basi tuandikie hapa chini.

Biashara njema na tukutane katika makala nyingine.